Wito umetolewa kwa wazazi humu nchini kuwa karibu na wanao kwa kuwapa ushauri nasaha kama njia mojawapo itakayosaidia kurejesha nidhamu miongoni mwao.
Akihutubu kwenye hafla ya mazishi ya Godwin Barasa eneo la Muyekhe eneobunge la Kabuchai mwekahazina wa muungano wa kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET kaunti ya Bungoma Bi Rebbeca Masibayi amesikitikia kisa kimoja mjini Kisii ambapo mwanafunzi anadaiwa kuwashambulia walimu kwa kisu na kuwaacha na majeraha.
Aidha Bi Masibayi amewashauri wazazi kuwapa wanao mwelekeo ulio bora ili kujitenga na visa vya maadili potovu.
Ametumia fursa hiyo kuwahimiza wazazi kuhakikisha wanao wanarejea shuleni ili kuendelea na masomo akihoji kuwa serikali itagharamia karo yao.
story by Richard Milimu