Naibu Kamishna kaunti ndogo ya Cheptais eneo bunge la Mlima Elgon kaunti ya Bungoma Samuel Towet amesema ipo haja kwa jamii za eneo hilo kushirikiana ili kumaliza utata unaohusu usambazaji maji safi kwa wakazi.

Akizungumza wakati wa mkutano wa uhamasisho kuhusu matumizi ya maji safi kwa wakazi, Naibu kamishna huyo amesema ni haki kikatiba kwa kila mkazi kupata maji safi na vilevile kuyatumia vyema

Naye msaidizi wa Kamishna eneo hilo Boaz Koecha akiwahakikishia kuwa serikali tayari imeanzisha mipango ya kumaliza uhasama uliopo kuhusu usambazaji maji safi katika eneo hilo la Cheptais na eneo la Mlima Elgon kwa jumla

Kuhusu usalama, Kamanda wa Polisi eneo hilo Mwita Marwa amesema polisi wanaendeleza doria kuimarisha usalama hasa baada ya kuripotiwa visa kadhaa vya ukosefu wa usalama ikiwemo uvamizi na wizi katika siku za hivi maajuzi.

story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE