Mwenyekiti wa muungano wa watu wenye ulemavu kaunti ya Busia Ronald Obiero amewasuta maafisa waliosimamia zoezi la kuwasajili makurutu wa kujiunga na shirika la wanyama pori nchini KWS kwa kuwapuuza walemavu kwenye kaunti hiyo.

Kwenye kikao na wanahabari mjini Busia, Obiero amedai kuwa zoezi hilo ambalo lilifanyika hivi majuzi lilikumbwa na visa vya udanganyifu na kuwanyima nafasi walemavu.

Obiero aidha amelalamikia shirika hilo la KWS kwa kutoa nafasi moja pekee kwa walemavu licha ya kaunti ya Busia kuwa na idadi kubwa ya walemavu.

Jumla ya watu 86 walichaguliwa wakati wa zoezi hilo lililofanyika Jumanne wiki hii, wakiwemo wanaume 60 na wanawake 26 miongoni mwao mlemavu mmoja wa kike.

Kwa mujibu wa Jacob Mwanzala msimamizi wa zoezi hilo, mpango huo wa uteuzi wa makurutu ulifanyika kwa njia ya uwazi kinyume na madai ya watu wenye ulemavu.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE