Serikali ya kaunti ya Busia imekamilisha zoezi la kupokea maombi kutoka kwa watu wanaotaka kuajiriwa Kama wahudumu wapya wa afya ambao watahojiwa na kuajiriwa na serikali ya gavana Sospeter Ojaamong kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wahudumu wa afya wanaoshiriki mgomo.

Naibu gavana wa Busia Moses Mulomi amesema hawatafunga hospitali na zahanati na kuacha wagonjwa kuhangaika kutokana na ukosefu wa wahudumu wa afya ilhali kaunti ya Busia ina wahudumu wa afya wengi ambao hawana ajira.

Amesema haya katika kituo cha afya cha Matayos kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa chumba cha X-ray cha kituo hicho, huku akiungwa mkono na afisa mkuu wa idara ya afya Jonathan Inno aliyeandamana naye akisema  serikali ya Busia imetimiza matakwa ya wahudumu wa afya yanayowapaswa kufanywa chini ya serikali ya kaunti. 

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE