Hali si hali katika eneo la Kapedo ambapo oparesheni ya kuwakamata wahalifu bado unaendelea, japo askofu la kanisa la Katoliki jimbo la Eldoret Askofu Dominic Kimengich ametoa mapendekezo kuhusiana na suala hilo na kusema kuwa idara ya usalama inafaa kuwakamata wahalifu pekee bali si kuathiri wakazi kutoka eneo hilo.

Vile vile ameongeza kuwa licha ya jamii hizo kuwa wafugaji ameshauri serikali kuendeleza maendeleo mahali pale kwa kujenga barabara na shule ili wapate elimu bora na waweze kuepuke na uhalifu.

Kando na hayo, Askofu Kimengich amezungumzia suala la shule za bweni kufungwa amesisitiza kuwa hakuna tofauti za shule bali wanafunzi wanafaa kujua maadili.

Hata hivyo jambo la kuwa na kasisi shuleni linafaa kuzingatiwa kwani itawasaidia wanafunzi kupata ushauri na mafunzo kamili kuhusiana na maadili. 

Story by Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE