Mwanaume mwenye umri wa makamo kwa majina Shikuku Cheto amefariki kutokana na ajali ya barabara iliotokea katika barabara  ya Malava kuelekea Webuye baada ya trekta waliyokuwa nayo kukatika breki na kumkanyaga katikati mwa tumbo lake na kupoteza uhai kabla hajafikishwa hosipitalini

Akizungumza na idhaa hii  nduguye marehemu julius fulani amehoji kuwa lori lilifeli lilipokuwa likipanda mlima kisha aliporuka ili aweke mawe ya kuzuia kurudi nyuma akateleza na kuanguka.

Kulingana na shemejiye Hellen Daniel amesema kuwa amesitikishwa na tukio hilo huku akihoji kuwa huenda kuna njama ya kupoteza uhalisia wa kifo hicho.

Aidha familia hiyo ikiongozwa na naumi Peter imeiomba serikali kuingilia kati na kuwasaitia.

Hata hivo chifu wa kabras mashariki Musa Batete amedhibitisha kisa hicho na kuhoji kuwa mwili wa mwenda zake umepelekwa katika chumba cha kuifadhi wafu cha hosipitali ya Kakamega.

Batete pia ametumia fursa hiyo kuwarai wamiliki wa magari kuyarekebisha magari yao kabla hawachayapeleka barabarani ili kuzuia maafa zaidi.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE