Familia moja kutoka kijiji cha Musasa kata ya Shiveye eneo bunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega inaelezea kunyanyaswa na mkaaazi mmoja eneo hilo anayedaiwa kutokamilisha kiwango cha pesa ambacho waliagizana wakati wa kununua shamba ambalo wanamoishi kwa sasa jambo ambalo wanalitaka ofisi za kutetea haki za kibinadamu kuingilia kati na kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

 Familia hiyo ikiongozwa na Charles Kanganyia inaelezea kuwa tangu kufariki kwa babake James Kangayia mnamo mwaka wa 2009 wamejaribu kila wawezalo ili deni lao liwe linalipwa ilhali imekuwa ngumu 

 Aidha wanaelezea kuwa licha ya wao kuzingatia masharti  ya koti   ili shamba lao liwe linarudi hali imekuwa vuta ni kuvute jambo ambalo kwa sasa wanalisuta vikali na kutaka waelezwe ni  njia ipi ilitumika kumaliza mgogoro huo 

“Baba yangu aliuzia Timona Amukombi shamba shilingi elfu sita mwaka wa 1976 na wakaandikishana atlipa polepole. Wakati baba yangu alikufa mwaka wa 2009 alituambia kwamba Timona ako na deni na kama awezi lipa asiishi kwa hiyo shamba. Na sasa Timona alikufa mwaka wa 2019 tukaita familia yake tukae tuelewane wakakataa sasa tunataka wale ambao wanasimamia maswala ya shamba na haki za kibinadamu waingilie kati watusaidie kusuluisha huu mzozo kwa saababu tumekua kotini lakini bado hakuna manufaa.” Familia ilielezea

 Akizungumza baada ya kutokea kwa mvutano huo naibu chifu wa eneo hilo amekashifu hatua ambayo imechukuliwa kuzuia kuzika kwa mwili wa marehemu ambaye anasemekana kununua shamba hilo akiendelea kuwasihi familia ya Charles Kangayia kuwachilia mwili ukatolewe hospitali ya Rufaa ya Kakamega ukazikwe jambo ambalo limeungwa mkono na wale wanaodaiwa walipe hela hizo.

 Story by Shitemi Boaz

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE