Mzozo wa uongozi katika bunge la kaunti ya Kakamega unazidi kutokota hii baada ya jumla ya wakilishi wadi 69 kati ya 89 wa bunge la kaunti ya Kakamega wamemtimua kiongozi wa wengi Joel Ongoro kutoka kwa wadhfa huo na pia kumuondoa kwa bodi ya bunge hilo kwa madai ya ubadhirifu wa fedha na kushindwa kushughulikia ipasavyo maslahi ya wakilishi wadi hao kwa bodi
Wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari muda mfupi tu baada ya uamzi huo, wakilishi wadi hao wakiongozwa na Bonface Akosi wa Esumeyia/Shikomari, Farouk Machanje wa Isukha Kusini, Walter Andati wa Butsotso kusini wamesema uamzi ambao wakilishi wadi hao waliafiki kwa majengo ya bunge sio kwa mirengo ya vyama wakitaja ubadhirifu wa fedha na kutowakilishwa vyema katika bodi ya bunge hilo kama baadhi ya madai ya kumuondoa kiongozi wa wengi Joel Ongoro kwenye wadhifa huo
Kwa sasa wakilishi wadi wamemchagua Charles Imbali wa Idakho ya kati kuwawakilishi katika bodi ya bunge hilo na Paul Ashiachi Wanda wa wadi ya Musanda kuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo huku wakishikilia kwamba hawakubali kushinikizwa na mtu wa nje ya bunge hilo kubadili uamzi huo
Hata hivyo kiongozi wa wengi anadaiwa kutimuliwa kutoka kwa wadhfa huo Joel Ongoro kupitia kwa njia ya simu amepuzuulia mbali uamzi wa viongozi hao na kusema kuwa uamzi huo hujafuata sharia
Story by Richard Milimu