Kama moja wapo wa njia za kuzuia msambao wa corona mahakama ya Busia imeanzisha mpango wa kuendesha shughuli za kusikiza kesi kupitia njia ya mtandao

Akiongea na waandishi wa habari mjini Busia hakimu mkuu wa mahakama ya Busia Lucy Ambasi amesema kuwa wameunganisha gereza la Busia pamoja na vituo vinane vya polisi kaunti hiyo kwa njia ya mtandao huku washukiwa wakisomewa mashtaka dhidi yao bila kufikishwa mahakamani.

Ambasi amesema kuwa hatua hiyo imenuia kupunguza msongamano katika mahakama ya Busia na kuhatarisha maisha ya wenyeji ikizingatiwa kuwa hamna nafasi washukiwa kurundikana kwenye seli mbali na idadi ya watu wanaohudhuria kufuatilia kesi zao.

Aidha bi Ambasi amesema kuwa washukiwa wenye makosa madogo waachiliwa kwa dhamana huku wengine wakipewa adhabu ya kuhudumia jamii.

Wakati uo huo bi Ambasi amefichua kuwa mpango huo utarahisisha wenyeji wa kaunti hiyo kufuatialia kesi zao wakiwa mahali popote bila kulazimika kusafiri.

Mwenyekiti wa chama cha mawakili kaunti ya Busia Joseph Makokha amesema kwamba licha ya mfumo huo kuwa na manufaa kuna haja kwa mahakama kubuni mbinu mbadala ya kuskiza kesi hasa kwa wazee.

Wakati uo huo amempongeza jaji mkuu Martha Koome kwa hatua ya kutuma majaji wa mahakama ya rufaa mjini Kisumu kwa kile amekitaja kama njia ya kupunguza mrundiko wa kesi za rufaa.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE