Serikali ya kaunti ya Vihiga imetumia takriban shilingi milioni 150 kwa kipinda cha miaka mitatu ambacho kimekamilika kwa juhudi za kuimaririsha na kuulinda msitu uliyoko kwa vilima vya Maragoli katika eneo bunge la Vihiga 

Akizungumza muda mfupi tu baada ya kuzuru msitu huo, gavana wa kaunti ya Vihiga Wilber Ottichilo amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa msitu huo unalindwa na unarejelea hadhi yake jinsi ilivyokuwa hapo awali 

Juhudi za kuulinda na kuifadhi msitu huo ambazo zinafanywa na serikali ya kaunti hiyo zimezaa matunda ambapo kiwango cha upanzi wa miti kwenye msitu huo kimeongezeka kutoka asilimia 4% hadi asilimia 14% kwa muda wa miaka mitatu iliyopita, huku gavana Ottichilo akitaka kuwepo kwa sheria maalum ambazo zitatumika kudhibiti uharibifu wa msitu huo 

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE