Ni sharti tume ya kuajiri waalimu inchni kuharakisha kuwapandisha vyeo waalimu walio hitimu kufanyiwa hivyo.
Akizungumza katika eneo bunge la Bumula kaunti ya Bungoma, mwenyekiti wa chama cha kutetea masilahi ya walimu wa shule za msingi Bungoma Mashariki Agrey Namis,i amesema kuwa tume ya kuajiri waalimu huchukua muda mrefu kupandisha walimu walio hitimu katika viwango tofauti kulingana na masomo waliyo nayo.
Namisi pia ametaka mgurugenzi mkuu wa tume ya kuajiri waalimu nchini Nancy Macharia kudhibitisha sitakabadhi za walimu hao wanao sitahili kupandishwa vyeo, na amesema sharti hilo litekelezwe chini ya miezi sita’ ‘
Aidha Namisi amelipinga moja kwa moja swala la waalimu kutakiwa kuwa na diploma pekee bali si kuwa na shahada kutoka katika chuo kikuu huku akisema kuwa itaathiri waalimu wa shule zaupili pakubwa.
By Hillary Karungani