Viongozi wa makanisa ya Kibaptisti eneo la Kakamega ya kati wameungana na wenzao kote nchini kukashifu hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kuongeza muda wa kufungwa kwa makanisa
Wakiongozwa na mwenyekiti wa makanisa hayo eneo la Butsotso ya Mashariki Andrew Chepkosia wamesema wako tayari kuzingatia masharti yaliyowekwa wakati wa ibada
Vile vile mchungaji Chepkosia ameitaka serikali kuendeleza msaada kwa wakongwe na wasiojiweza wakati huu wa janga la corona
By Lindah Adhiambo