Katibu mkuu wa chama cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Busia Moffat Okisai amelisuta vikali baraza la mitihani nchini KNEC kwa kuchelewesha malipo ya walimu ambao walisahihisha mitihani ya kitaifa ya mwaka jana huku baadhi ya walimu hao wakiendelea kukabiliwa na wakati mgumu.

Okisai ameelezea kusikitishwa kuwa licha ya walimu ambao walijitolea kusahihisha mitihani ya kitaifa haswa ya KCSE kutumia fedha zao katika shughuli za kusafiri na mahitaji mengine baraza hilo limedinda kuwalipa pesa zao na sasa wengi wanaishi kwa madeni.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Busia katibu huyo ameelezea kuhofia kuwa huenda walimu wengi wakasusia kujihusisha na usahihishaji wa mitihani ya kitaifa katika miaka ijayo huku akitoa changamoto kwa barabaza hili kuiga mfano wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE