Maafisa wa polisi wa kituo cha Lumakanda eneo bunge la  Lugari kaunti ya Kakamega  wanamzuilia mwanamume mmoja kwa tuhuma za kumdunga kisu na kumuua rafikiye baada ya kumshuku kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe katika kijiji cha Lukhuna kata ndogo ya mbagara…

Akithibitisha kisa hiki Kamanda wa polisi katika eneo bunge la Lugari Bernard Ngungu amesema wawili hao walikuwa wafanyikazi katika boma la Henry Miwani ambapo ugomvi uliibuka baina yao baada ya mmoja wao kumshuku mwenzake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe kabla ya kumdunga kisu na kumuua papo hapo.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo mshukiwa alijaribu kutoroka kabla ya kunaswa na wananchi na kukabidhiwa kwa mafisa wa polisi.

Ngungu amesema mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Lumakanda huku uchuguzi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.

Maiti ya mwendazake iliondolewa na kupelekwa katika hifadhi ya wafu ya kimbilio katika kaunti jirani ya Uasin Gishu.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE