Siku 40 za ukumbusho wa aliyekuwa mtangazaji wa kituo hiki cha 102.2 Lubao FM Tom Cliff Makanga zimeandaliwa leo nyumbani kwao Muraka eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega huku familia,ndugu,jamaa,marafiki,mashabiki na watangazaji wenza wakijumuika nyumbani kwao kusherehekea siku hii muhimu na kuifariji familia

Watangazi wenza wakimtaja marehemu Tom Cliff Makanga kama mtangazaji shupavu,mwalimu mwema na mtiifu kazini na hivyo kukosekana kwake kukiwa pigo kubwa hadi sasa hivi

Tomcliff we really miss you, you were displine smiling always today i realize you to rest in peace and pray for us to stay in peace as you wanted people to be. tunakumiss kwa ile kona tulikua tukikaaa tukifanya news rest in Peace Tomcliffe

Babake na mamake Tom cliff wakielezea masikitikio yao baada ya kifo hicho na kuwapongeza wote waliowasaidia wakati msiba ulipotokea haswa usimamizi wa kituo hiki chini ya afisa mkuu mtendaji Fredrick Witaba, meneja Charles Oduor na mkurugenzi wa kifedha Steven Witaba Shisia

Nao ndugu wa marehemu Tom Cliff Makanga pia wakimwomboleza ndugu yao na kuelezea pigo walilopata kwa baadhi wakisema ni kidonda kisichopona haraka 

Nao mashabiki wa kituo hiki wakifika pia kufariji familia ya mtangazaji aliyeenziwa Tom Cliff Makanga 

By Sajida Javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE