Mwanamme mmoja wa kadri ya miaka 27 kutoka kijiji cha Mayuge eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega amepagawa kwa njia tatanishi baada ya kudaiwa kuchumbia kidosho  kinachoaminika kuwa jini na kisha kubadilika kuwa mbuzi iliyo na pembe sawia chupa ya soda.

Joel Namasaka anasema alikutana na msichana mrembo sehemu ya Soy eneo bunge la Likuyani akidhania amekutana na mrembo wa kuoa ila alipoenda naye hadi nyumbani kwao akabadilika na kuwa mbuzi kupelekea kwake kupagawa kighafla.

Babake mwathiriwa Peter Wawire Namasaka na jiranie Loice Mulanda wanasema mwathiriwa aliwaeleza kuwa alipokutana na mrembo huyo aliamua kumnunulia soda mbili na mkate ambazo alitumbikiza kwa mdomo mara maoja na kumaliza, na sasa wamelazimika kumfunga mwanao kwa kamba amekuwa akiharibu vitu kama vile kuteketeza nguo, nyumba yake kati ya zingine.

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE