Kamanda wa polisi kaunti ya Homabay Esther Seronei amewataka waanga wa dhulma za kijinsia kuripoti visa hivyo kwa polisi ili hatua za dharura zichukuliwe
Seronei amehoji kuwa baadhi ya watoto wakiwamo wavulana na wasichana wanadhulumiwa ila visa hivyo huishia nyumbani tu huku waathiriwa wakikosa kupata haki
Naibu kamishana wa kaunti ndogo ya Awendo Mary Wamalwa kwa upande wake ameridhia idadi ya watoto wanazidi kujiunga na kidato cha kwanza kaunti hiyo akiwataka wazazi kuwaruhusu hata waliojifungua kurejea shuleni
By James Nadwa