Vyongozi wa serikali kuu kaunti ya Bungoma wamejitokeza kupiga vita ndoa pamoja na mimba za mapema miongoni mwa watoto wa kike eneo hilo

Kamishana wa Bungoma Samwel Ekimiti amewaonya wanaohusika kuwaoza watoto wa umri mdogo kuwa wataandamwa na mkono wa sheria huku akiwataka machifu na manaibu wao kuhakikisha kuwa wanawatia nguvuni wahusika

Kwa upande wake naibu kamishana wa kaunti ndogo ya Bungoma West Henry Katana amesikitikia ongezeko la visa vya  mimba za mapema eneo hilo akilaumu mfanyibiasha mmoja ambaye hakumtaja kama baadhi ya wanaondeleza dhulma hizo akisema kuwa sheria itafwata mkondo wake.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwanaharakati wa maendeleo kaunti ya Bungoma Swine Khayanga  aliyewataka wazazi kuwa makini na  kuchunguza mienendo ya watoto wao kama njia pekee ya kukabili tabia potovu miongoni mwao

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE