Hulka ya kubagua kazi imekuwa chanzo Cha ukosefu wa kazi miongoni mwa vijana Kanda ya magharibi
Hii ni kauli yake mwanasiasa kutoka wadi ya MARAMA North eneobunge la BUTERE Charles Etemesi
Akizungumza na kituo hiki Etemesi amewataka vijana kutobagua kazi kama njia pekee ya kupigana na tatizo hilo la ukosefu wa ajira eneo hilo
Etemesi aidha ametilia shaka juhudi za MCA wa sasa katika kuboresha viwango vya masomo ambavyo anadai vimedorora pakubwa
Kiongozi huyo ameonekana kushabikia mdahalo wa kuwataka wanasiasa vyongozi kuwa na degree akisema kuwa hili litaimarisha uongozi mashinani
By James Nadwa