Illustration on theme big colored set different types of syringes, needles for hospital. Syringe consisting of collection accessory with quality control needle. Needle in syringe main medicine symbol

Familia moja kutoka kijiji cha Budonga eneo bunge la Navakholo inaomba msaada wa kugharamikia upasuaji wa uvimbe katika kichwa cha mwano wa miezi minane baada ya kushindwa kupata zaidi ya elfu kumi zinazohitajika hospitalini. 

Rachel Mboya mamake anasimulia kwa huzuni kwamba mwanawe alianza kuwa na uvimbe kichwani miezi miwili baada ya kujifungua na alipopelekwa hospitalini akaarifiwa kuwa mwanao alikuwa na ugonjwa wa kujaa maji kichwani na anahitajika kufanyiwa upasuaji kuyaondoa.

Wanasema kwamba mtoto huyu anateseka kwa mauvimu haswa nyakati za usiku hali inayowalazimu kukesha usiku ili kushughulikia na ombi lao la kumwona akiwa amerejelea hali yake ya kawaida ni ndoto.

Familia hio ambayo inategemea vibarua vya kila siku angalau kupata chakula inasema haina uwezo wa kugharamikia matibabu ya mpendwa wao ambapo sasa inaomba wahisani na viongozi wa eneo hili kuwasadia kumtibu mwanao ili aweze kuendela na maisha ya kawaida

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE