Idadi ya watoto ambao wametolewa kupokezwa chanjo ya ukambi katika kaunti ndogo ya Lurambi imekuwa ya chini mno tangu zoezi hili kung’oa nanga kwa juma moja sasa
Afisa wa kuimaisha afya kaunti ya Kakamega Lorna Mumia amezuru baadhi ya vituo vya afya na kuelezea kuhusu zoezi hili
Amewataka wazazi kutumia siku mbili zilizosalia kuona kwamba watoto wao wanapata chanjo kabla ya shuguli hii kukamilika siku ya Jumatatu akisema chanjo ni muhimu kwa kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi
By Linda Adhiambo