Baadhi ya wenyeji wa budalang’i hasa wavuvi na makundi ya kuhifadh mazingira wameelezea kuhofia kuzuka kwa aina mpya ya gugu maji ambalo huenda ikalemaza shughuli za uvuvi na usafiri mbali na kuharibu mazingira.

Wakiongozwa na Edwin Onyango na Khamala Wanjala wamesema kuwa kufuatia masaibu ya mafuriko ambayo wenyeji wanakabiliana nayo kila mara hasa vijiji vya chemichemi za yala wanategemea maji kusafiri japo gugu hilo limetabaka kote na kufunika njia wanazotegemea.

Aidha wanahofia kuwa gugu hilo ambalo kwa sasa limevamia maeneo ya kadhaa ya wadi ya Bunyala Kusini linasambaa kwa haraka zaidi na huenda likawa kidonda sugu iwapo litaingia katika ziwa Victoria.

Wenyeji hao kwa sasa wanatoa wito kwa serikali ya kaunti ya busia na ile ya kitaifa kuingilia kati na kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na gugu hilo ili kutafuta suluhu la kudumu.

Wakazi hao wanahofia kuwa huenda gugu hilo likawa na madhara kwa afya zao kwa kuwa wanategemea maji hayo kwa matumizi ya nyumbani.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE