Mbunge wa Khwisero kaunti ya Kakamega Christopher Aseka na wakazi wa eneo hilo wamelalamikia ongezeko la visa vya ubakaji na mimba za mapema eneo hilo.

Akihutubia wakazi wa eneo hilo Aseka amesema visa vya mimba za mapema vimeongezeko akisema vinatokana na visa vya ubakaji akivitaka vitengo vya usalama kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika.

Ni jambo liloungwa mkono na wenyeji chini ya Edward Oluchiri ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha kanu kaunti ya Kakamega, anayesema visa hivyo vinapelekea wenyeji hasa wajane kuishi katika hali ya wasiwasi hasa nyakati za usiku.

By Linda Othiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE