Wanaharakati wa kisiasa Kaunti ya Bungoma chini ya vuguvugu la Bungoma Liberation sasa wanamtaka Gavana wa Kaunti hiyo Wycliffe Wangamati kujitokeza wazi kuelezea jinsi serikali ya Kaunti hiyo ilivyotumia mgao wa fedha za kukabili msambao wa virusi vya Korona.

Kwenye taarifa kwa wanahabari, Isaiah Sakonyi ambaye ni msemaji wa vuguvugu hilo, ameikosoa serikali ya Kaunti kufuatia ongezeko katika ufisadi, siku chache baada ya ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali kuiratibu Kaunti ya Bungoma miongoni mwa Kaunti zilizotumia vibaya mgao wa pesa za kukabili janga la Covid-19.

Huu ni wakati wa mwisho wa watu wanao jitakia, watu wanao fuja pesa za umma. tumesikia na pia tumeona kwa TV vile watu wanakula tu pesa ya umma. tumeona kaunti ya Bungoma imekuwa short listed na kuwa namba mbili kwa matumizi mabaya ya pesa za corona na inafaa tukomeshe

Wakati uo huo, wanaharakati hao wameilaumu serikali ya Kaunti kwa kuwahangaisha wapinzani wake ikiwemo kuwatia mbaroni bila sababu za kimsingi.

Huyu dada yetu ameshikwa juzi ametukaribisha kule Namwela kwa wadi yake kwenda huko kusaidia akina mama wajane na wasiojiweza katika ugavi wa mbegu under Zakari Barasa Panda Mbegu initiative sasa ndio maana wameanza kumuindimidate ndio aogope asitembee na timu ya Zakari Barasa. This is the main reason, hizi vitu zingine ambazo ni social media ni ukora tu, there is nothing substancial.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE