Muungano wa kitaifa wa wauguzi nchini wa ‘Kenya Progressive Nurses Association’ umeitaka serikali kuu na zile za kaunti kutumia fedha ambazo hupata kwa wahisani wa nje kwa kuegeza pakubwa kwenye vyumba vya kuwalaza wagonjwa mahututi haswa kwenye mitambo ya kuhifadhi na kutoa hewa safi (oxygen) ili  kukabili uhaba uliyopo wa hewa hiyo nchini

Akizungumza mjini Kakamega, mwenyekiti wa muungano huo nchini Michael Nyongesa, amesema kutokuwepo  kwa mpangilio maalum kwenye matumiza ya fedha za humu nchini umechangia nyingi ya hospitali za humu nchini kukosa kukabiliana na dharura ya janga la korona

Haya yajiri baada ya waziri wa afya kaunti ya Kakamega Collins Matemba kusema kuwa kaunti hiyo imejianda vilivyo kuona kuwa kuna hewa ya oksijeni kwa hospitali za eneo hilo

Hata hivyo Nyongesa amedokeza  kuwa muungano huo uko tayari kushirikiana na serikali za kaunti kuhusiana na swala hilo  iwapo watapewa nafasi

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE