Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Otonglo kwenye barabara kuu ya Kisumu –  kisiani siku ya jumatano ambapo mwili ya mwanamume wa miaka thelathini na tatu ulipatikana kwenye gari lililokua limeegeshwa kando ya kituo cha mafuta.

inaripotiwa kwamba Habel Oile alikuwa ameegesha gari katika kituo cha mafuta ambapo walinzi wa usiku waligundua kwamba alikaa kwa gari kwa muda mrefu.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya kisumu Samuel Anampiu alisema kwamba mmoja wa walinzi alikaribia karibu na gari hilo na kuchungulia ndani na kuona mwanamume akiwa amelala kiti cha mbele.

Aliwajulisha polisi ambao walifika baada ya masaa machache na kuingia kwenye gari hilo na kugundua kwamba alikua amefariki.

kamanda wa polisi Anampiu alisema kwamba maafisa hao walipata chupa yenye milimita ishirini na tano ya dawa ya wadudu wakidhania kuwa hicho ndicho chanzo cha kifo chake.

Maafisa walichukua chupa hio na kuitumia kama chombo cha chanzo cha upelelezi.

mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya kaunti ya Kisumu.

By Winnie Akinyi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE