Lubao FM | 102.2 Hz

Mwanafunzi wa Nne Bora nchini katika matokeo ya mtiani wa kidato cha nne mwaka huu kaunti ya Kakamega

Ilikuwa furaha kwa familia ya bwana na bi Morias kutoka kaunti ya Kakamega baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne kutangazwa naye waziri wa elimu profesa George Magoha.

Mwana wao Morias Bob Ong’are aliyekua akisomea shule ya upili ya Alliance jijini Nairobi,  aliweza kuibuka wa nne bora katika taifa la Kenya na aliweza kudhihirisha furaha yake katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo hiki licha ya kutotarajia kuliongoza taifa kwa nambari ya nne

Bob alieleza kuwa siri ya kufaulu katika majiribio ni kutia bidii, kumtanguliza Mungu na kubwa zaidi kuwaheshimu wazazi

Mamake Bob, Doris Morias, pia aliweza kudhihirisha furaha yake baada ya mtoto wake kufanya vyema katika mtihani wa kitaifa huku akiwasihi wazazi wazidi kuwahimiza wanao kupenda elimu

By Tomcliff Makanga

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE