Wakaazi katika kaunti ya Kakamega wamelalamikia huduma duni kwenye afisi za ardhi huku wakitoa wito kwa serikali kufanyia mabadiliko usimamizi wa idara hiyo muhimu kwani wengi wao wameshindwa kupata stakabadhi hitajika za mashamba yao kutokana na ufisadi.
Wakizungumza nje ya afisi hizo mjini Kakamega wenyeji hao wakiongozwa na Noordin Miheso wanadai kuwa kila mara wanapotafuta huduma kwenye afisi hizo wanapitia changamoto nyingi huku wakitumwa kutafuta huduma hizo nje ya afisi ambapo pia wanakosa stakabadhi hitajika za mashamba yao .
Ni kauli iliyotiliwa mkazo na baadhi ya wenyeji akiwemo Joseph Owino Muchesia huku wakimtaka rais Uhuru Kenyatta na gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya kuingilia kati kuwasaidia wenyeji ambao wengi wao wameishi miaka mingi kwa kushindwa kupata huduma kwenye afisi hizo.
Juhudi zetu za kupata wahusika kupata usemi wao ziliambulia patupu .
By Richard Milimu