Afisa mkuu wa makarani aliyekamatwa na kushtakiwa siku ya Jumatano kwa kuchukua hongo katika Sheria House.
Ya’qub Abubakar Omar alishtakiwa tarehe 10 mwezi September 2019, kwa kuchukua hongo yenye kiasi cha shilingi 2,500 kutoka kwa Calistus Wilunda.
Imearifiwa kuwa hicho ndicho kiasi cha pesa alichoomba ndiposa aweze kutoa cheti cha kuzaliwa binti wa Wilunda.
Kisa hiki kinasemekana kilitokea katika kituo chake cha idara ya madai.
Mara ya pili, inasemekana alishtakiwa kwa kupokea hongo yenye kiasi sawia na aliyoichukua mwezi septemba 2019.
Hata hivyo aliomba kwamba hana hatia mbele ya chifu wa chama cha kupambana na ufisadi Douglas Ogoti.
Omar aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki mia moja na Kesi itasikilizwa tarehe 25 mwezi mei 2021
By Marseline Musweda