Shule ya upili ya Isongo wilayani Mumias Mashariki imeimarisha matokeo ya mwaka huu huku shule hiyo ikipata alama ya wastani ya 6.2 ikikinganishwa na 4.00 ya mwaka ulopita 
Quintine Wambani, Naomi Omoto na Frederick Malala waliongoza msururu wa wanatahiniwa hao kwa kuzoa alama 63.04, 63.03 na 63.00 mtawalia 

Akizungumza na kituo hiki afisini mwake mwalimu mkuu wa shule hiyo David Wafula amesema kuwa hii ni kutokana na mikakakti waloweka licha ya changamoto ya ugonjwa wa Corona
Wafula amesema kuwa Kati ya watahiniwa 73 waoukalia mtihani huo 10 walipata alama ya B huku 20 kati yao wakipata nafasi ya moja kwa moja kungia chuo kikuu
Kwenye shule jirani ya Lubinu boys, watahiniwa 182 kati ya 232 waloukalia mtihani huo  walipata alama ya B huku zaidi ya 200 wakipata nafasi ya moja kwa moja kujiunga na vyuo vikuu.  

By James Nandwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE