Kwenye kikao na wanahabari ofisini mwake Askofu wa kanisa hilo Joseph Wandera amesema kuwa kama kanisa hawakubaliani kwa vyovyote vile na ghasia haswa za Matungu na kuwataka vyongozi kuwajibika
Wandera aidha ametaka adhabu kali kutolewa kwa wahusika kama njia mojawapo ya kudhibiti vitendo hivyo
Kwa upande wake msemaji wa wahubiri eneo la Matungu Patrick Obonyo ameelekezea kidole Cha lawama polisi akiwataka kama walofanikisha vitendo hivyo
Haya yanajiri huku waziri Matiangi akitoa onto kwa wanasiasa wenye hulka ya kuzua ghasia wakati wa uchaguzi kwamba chuma Chao ki motoni
Hata hivyo alilalama namna mahakama inavyoshugulukia kesi hizo na kuwaachilia wahusika kwa Bondi akihoji kuwa hili linachochea vitendo hivyo
Story by James Nadwa