Mwakilishi wadi ya Marama Magharibi eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega Boaz Milton Omukunde maarufu kama Saitama amewataka wakuu wa shule kuridhika na fedha za basari ambazo zimepeanwa kwa shule na kuwarusu wanafunzi kuendelea na masomo yao bila kutumwa nyumbani kila wakati


Saitama amesema hali ngumu ya masiha iliyosababishwa na corona imeathiri mapato ya wazazi na ni muhimu walimu kuwavumilia huku akifichua kuwa zaidi ya wanafunzi mia tano wamenufaka na usaidizi wa basari ya wadi


 Saitama ambaye ametembelea shule kadhaa kupeana usaidizi wa chakula wakati wa mitihani amewahimiza washikadau kujitokeza na kushirikiana kuboresha viwango vya elimu


By Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE