Wakaazi wa wadi ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon wametakiwa kuwa na subra huku serikali ya kaunti ya Bungoma inapoendelea kushughulikia swala la uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo kwenye wadi hiyo.

Akihutubu kwenye hafla ya mazishi eneo la Cheptais mwakilishi wadi wa eneo hilo bi Jane Chebet amedokeza kuwa tayari serikali ya kaunti ya Bungoma imetenga shilingi laki saba zitakazotumika kukarabati tanki la maji ambalo limekuwa likivuja maji na kupelekea wakaazi kukosa bidhaa hiyo muhimu.

Wakati uo huo bi Chebet mbaye ametangaza kugombea kiti cha ubunge eneo hilo amewahimiza viongozi  wa kisiasa kutoka Mlima Elgon kuhubiri amani ili kuunganisha jamii zote eneo hilo.

Amedokeza kuwa ukarabati wa baadhi ya barabara na daraja  eneo hilo unaendelea na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE