Shughuli ya kibiashara na uchukuzi katika barabara ya kutoka Shinyalu kuelekea eneo la Madala ambapo kiwanda cha chai kinanuiwa kujengwa katika eneo bunge la Shinyalu zilitatizika kwa muda baada ya wakulima wa chai kuandamana kushinikiza gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya kukamilisha mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho ili kuwaepushia masaibu wanayokumbana nayo kwa zao hilo
Wakizungumza nje la lango la ua linalozingira shamba ambalo kiwanda hicho kinanuiwa kujengwa walikulima hao wakiongozwa na Rose Yakhama na Shem Miheso Muhanji wanashangaa kuona muhula wa gavana Oparanya ukitamatika bila kutimiza ahadi ya kuwepo kwa kiwanda hicho tangu mwaka wa 2015
Wanasema kuwanda hicho cha chai kIlistahili kushughulikia zao la wakulima hao takriban alfu nne kutoka eneo la Shinyalu, Ikolomani na Khwisero
Ni swala ambalo limewaghabisha vijana ambao pia ni wakulima kutoka eneo hilo wakisema kuwa kutoendelea kwa ujenzi wa kiwanda hicho kunachangiwa na ufisadi kutoka kwa serikali ya kaunti ya Kakamega
Hata hivyo wakulima hao wamemtaka gavana Oparanya kupitia kwa wizira ya kilimo na viwanda ya kaunti hii kutimiza ahadi zake la si hivyo wanapania kuandaa maandamano
By Richard Milimu