Wasichana wapatao alfu sita walio chini ya miaka kumi na minane waliathirika na mimba za mapema katika eneo la Navakholo kaunti ya Kakamega mwaka jana huku idadi hiyo ikitarajiwa kuwa imeongezeka
Akiongea kwenye kikao cha kuwahamasisha washikadau kuhusu mimba za mapema na uavyaji mimba, muuguzi msimamizi katika hospitali ya Navakholo Benard Kinara amesema visa vya uavyaji mimba mashinani vinaendelea kwa sababu ya wakazi kutofahamu kuwa sheria inaruhusu utoaji mimba kwa misingi ya ki afya
Msaidizi wa kamishona wa taarafa ya Navakholo Joshua Mutisya amewaonya viongozi wa mashinani wakiwemo nyumba kumi na maguru ambao watapatiaka wakifanya vikao vya kusuluhisha kesi za mimba kwa wasichana wa shule katika maboma
Mutisya vile vile amewasuta baadhi ya wazazi kwa kuwaficha watoto ambao wameathirika na kutatiza kesi kuendela akisema i wanachangia ukosefu wa haki kwa wasichana ambao wanadhulumiwa kimapenzi
Shirika la kijamii la Bumulusi ambalo liliandaa kikao hicho kupitia kwa Pamela Wambongo linaitaka serikali na wahisani kujitokeza na kuwasaidia kujenga kituo cha kuwasaidia waadhiriwa wa dhuluma za kijinsia na za kimapenzi kwani imekuwa vigumu kuwashughulikia
By Richard Milimu