Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Indangalasia wadi la Butsotso Mashriki kaunti ya Kakamega ambaye alipoteza maisha kwa ajali ya trela ya miwa amezikwa nyumbani kwao kijiji cha Shianda huku wakazi wakiitaka serikali kuingilia kati kuekebisha hali ya usafirishaji miwa na trella za kampuni za miwa
Kupitia kwa mchungaji Apunza Indakwa wa kanisa la KAG wamesema trella miwa huendeshwa kwa njia mbaya na pia miwa inapangwa kwenye trella kwa njia ya kuhatarisha maisha ya watumizi wengine wa barabara
Wanaitaka kampuni ya West Kenya kufuatilia na kuona kwamba dereva wa trakta iliyohusika kwenye ajali hiyo na kutoweka anakamatwa na kushtakiwa
Walimu na wanafunzi pamoja na wasimamizi wa shule ya Indangalasia wakiongozwa na mchungaji Charles Omanyo walielezea huzuni yao kumpoteza mwanafunzi huyo ambaye alikuwa tegemea kwa matokeo bora masomoni
Kwa upande wake msimamizi mradi wa masomo wa jisimamie Elimu Initiative katika wadi ya Butsotso mashariki Cyrus Akhonya amewahimiza wazazi na washikadau kushirikiana kukuza shule za mashinani kwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wenye alama bora pia wanajiunga na shule hizo kuinua matokeo
By Linda Adhiambo