Mwanamume mmoja amemshtaki mamake katika mahakama ya Kakamega kwa madai kwamba anapanga kuwazuia kurithi mali ya baba yao aliyeaga ya jumla ya shilingi milioni 200.

Fami Idris ameiambia mahakama hiyo hii leo kwamba mamake wa kambo tayari alikuwa amebadilisha umiliki wa lori la kima cha shilingi milioni 7 kwa jina lake na nia ya kuwadhulumu.

Hata hivyo mamake anayetuhumiwa Zubeida Khasabuli, alikanusha madai hayo ya kujaribu kunyakua lori hilo kinyume na sheria mbele ya hakimu mkaazi Neolyne Akee.

Mama huyo ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 100, huku kesi hiyo ikiratibiwa kutajwa mnamo tarehe 21, juni mwaka huu.

Mali ambayo imeibua mzozo katika familia hii ilikuwa ya marehemu mfanyibiashara maarufu Idris Makokha, ambaye alikuwa akimiliki majumba ya kibiashara katika miji ya Kakamega, Bungoma na Mumias huku akijihusisha na biashara zingine tofauti.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE