Serikali imewaonya wazazi katika eneo la Navakholo watakao patikana wakifanyia biashara ya kimapenzi watoto wao hasa wasichana kujipatia pato

Msaidizi wa kamishona wa taarafa ya Bunyala Magharibi Moureen Kagwara amewataka wazazi kuwajibikia jukumu lao la kuwalinda watoto la sivyo watachukuliwa hatua

Environment tunalelea watoto wetu sai ni tofauti sana na ile sisi tulilelewa ndani. Kuna wazazi ambao hawawezi kuongea na watoto wao. wanawaelekeza kufanya maovu na hivyo kama mzazi unamkosea mtoto wako. Sisi kama serikali tunajua ni jukumu la mzazi kumlea mtoto wake ipasavyo na kumuelekeza ipasavyo tukipata mtoto yeyote na mwenendo mbaya mzazi tunakuchukulia hatua za kisheria

Chifu wa kata ya Bunyala Magharibi John Wasike ameelezea jinsi baadhi ya wazazi wanawatumia watoto wao kuwahadaa wavulana na kisha kuwakamata na kuwatoza faini akisema tayari mzazi mmoja ametiwa mbaroni

Hatutaki mimba za mapema za kuendeleza kukua kwa hii area, na kuna wazazi ambao wanatumia watoto wao kupata pesa wanatuma watoto wao wasichana kwa nyumba ya wavulana na baadaye kuenda kuashika na kuwatoa faini. sahi tumeshika baba mmoja ambaye amekua na tabia hiyo ya kutuma msichana wake kwa mvulana alafu baadaye anaenda kuwashika na kutoza faini. najua huyu ni kama mfano kwa wengine na tabia hiyo itakoma. nataka tukomeshe mimba za mapema kwa area hii ikue kwa watoto wa primary school ama  secondry school.

Waliyasema haya katika shule ya upili ya Nderema baada ya kikao cha kuwahamasisha viongozi wa mashinani kuhusu mimba za mapema huku baadhi ya waliohudhuria wakiunga mkono vikao vya aina hii

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE