Watu wanne akiwemo muhudumu wa bodaboda wamefariki papo hapo huku wengine wakiuguza majeraha baada ya kugongwa na trela katika eneo la Mshitoyi kwenye barabara kuu ya kutoka Ekero kuelekea Buyangu mchana wa leo.

Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, dereva wa trela hiyo iliyokua  ikitoka Buyangu kuelekea Sabatia Ilipoteza mwelekeo na kugonga pikipiki mbili zilizokua zikielekea Sabatia na kisha kubingiria mara kadhaa.

Trella ilikosa mwelekeo na ikagonga watu wa pikipiki kisha baadaye ikarotate mara mbili na pia ikaumiza watu ambao walikuwa wanatembea kando ya barabara na wamekufa

Akidhibitisha ajali hiyo kamanda wa trafiki kaunti ndogo ya Butere Goerge Owour amewataka watumizi wote wa barabara kuwa waangalifu haswa wanapokaribia eneo hilo ili kuepusha ajali zaidi.

Tukue waangalifu wakati tunatumia barabara. Tuweze kuendesha magari kwa makini ili tuepuke ajali ma maafa barabarani. Tunao tembea barabarani tutembelee kando kabisa na tuhakikishe kwamba tuko salama Alieleza kamanda wa trafiki

Miili ya wanne hao inahifadhiwa katika chumba cha wafu cha Butere

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE