Wakulima wanao peleka miwa kampuni ya sukari ya nzoia wameshikwa wakiandamana kwenye mchezo wa paka na panya baada ya maandamano ya amani wakitaka mkurugenzi wa kampuni hiyo kuwalipa pesa zao za miwa ambazo zimekawiya kwa muda mrefu

Wengi wa wakulima hao wamesema kwamba hawajalipwa tangu mwaka wa 2019 walipo peleka miwa yao kwa kiwanda hicho hadi wa leo kwani maisha yamekuwa magumu  sana na hili janga la korona

Walisema walikuwa na imani na mkurugenzi wa kiwanda hicho wanjala makokha baada ya kuchukuwa kandarasi kwenye afisi lakini wameachwa na masaibu baada ya kukosa kutimiza ahadi zao wakiendelea kuumia na umasikini

Jack munialo ambaye ni miongoni mwa wale wakulima alisema kiwanda hicho kinadaiwa shilingi milioni 700 nao wafanyikazi wakidai bilioni mbili . Aliongezea akisema hawatachoka hadi walipwe pesa zao ambapo pia ni haki zao kama wakulima huku waziri wa kilimo peter munya akiagiza kiwada hicho kuwalipa wakulima hao kwa muda wa siku saba kwa bei iliyoboreshwa  

By Brian Kinyanji

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE