Wanachama wa kamati ya uhasibu katika bunge la kaunti ya Bungoma wamegadhabishwa na hatua ya mawaziri katika serikali ya kaunti hii kudinda kujiwasilisha mbele yake ili kujibu maswali kuhusu matumizi ya fedha za mwaka wa kifedha wa elfu mbili kumi na nane elfu mbili kumina tisa.

Wakiwahutubia wanahabari katika mkahawa mmoja mjini Chwele wakiongozwa na  mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwakilishi wadi ya Lwandanyi Tonny Barasa wanasema hata baada ya kamati hiyo kuwaarifu mapema mawaziri  hawajajitokeza  kujibu maswali yalioyoibuliwa na mkaguzi mkuu wa serikali.

Aidha Barasa anasema watalazimika kuweka ripoti hiyo kwa umma kabla kutoa mapendekezo kwa bunge la seneti ili hatua zichukuliwe kwa wale  watakaopatikana kufuja fedha za umma.

Naye mwakilishi wadi ya Ndivisi Martin Pepela akihoji kuwa watatumia mbinu zote ili kuhakikisha mawaziri hao wanafika mbele ya kamati hiyo.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE