Naibu kamishna wa kaunti ndogo ya Cheptais eneobunge la Mlima Elgon Samwel Towet amewapongeza wazazi na wa wakuu wa utawala kwa kuhakikisha wanafunzi wanarejelea masomo yao baada ya likizo ndefu iliyotokana na mkurupuko wa virusi vya corona.

Akihutubu kwenye hafla moja katika wadi ya Cesikaki eneobunge la Mlima eEgon Towet amesema kufikia sasa asilimia kubwa ya wanafunzi wamerejea shuleni, na kudokeza kuwa wanamalizia shughuli ya kusambaza madawati katika shule mbalimbali.

Aidha Towet amehoji kuwa kiini cha mkutano wa maji ulioandaliwa hapo jana ni kuwaelimisha wakaazi kuhusu sheria inayoangazia swala la maji.

Naye msaidizi wa kamisha eneo hilo Boaz Koech akisema kama serikali watahakikisha  suluhu inapatikana dhidi ya changamoto zinazowakumba wananchi.

Kamanda wa polisi eneo hilo Mwita Marwa akiwahakikishia wakaazi wa Chesikaki  usalama wa kutosha.

Story By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE