Mjane mmoja afurushwa na baba mkwe kutoka kwa boma lake katika kijiji cha Kapsirwa kaunti ya Uasin Gishu.

Kulingana na mjane huyo Agnes Maiyo amekiri kuwa baada ya kumzika bwanake amekuwa akiishi kwa hali ya wasi wasi kwani baba mkwe amekuwa akimtishia na kutafuta namna yeyote ili kuweza kumfurusha kutoka kwa boma lake japo alijaribu kuripoti kisa hicho kwa chifu lakini juhudi za kupata usaidizi hazikufua dafu baada chifu huyo kumlaumu kwa kuenda kuripoti kisa hicho kwa polisi bila ilani yake.

Hata hivyo mzee wa mtaa wa eneo hilo Kiptoo Chepkurui amesihi kuwa mgogoro huo Uliwashinda ilibidi kuchukua hatua ya kumtafutia usaidizi.

Polisi wanamsaka Baba mkwe kwa kutoweka baada ya kutenda kisa hicho.

Vile vile mtetezi wa haki za binadamu Kimutai Kurui amehimiza DC kutoka eneo la Ainabkoi kuhamasisha machifu wa eneo hilo jinsi wanafaa kushughulikia suala la wajane kwani wengi wao wamekuwa wakinyanyaswa.

Story by Sharon Lukorito

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE