Huku mchakato wa kupigia debe ripoti ya maridhiano na upatanishi (BBI) nchini ikiendelea kushika kasi, wananchi wa kaunti ya Kakamega eneo bunge la Malava katika wanaomba serikali kuwafikia na kuwapa nakala hizo ili waweze kujisomea na kuzielewa.
Wananchi hao wanasema kwamba bado hawaelewi kilicho ndani ya nakala hiyo iwapo kitawajali wafanya biashara wa ngazi za chini wakiwemo wa sekta ya boda-boda au la.
Hata hivyo wanaomba serikali kuweka kipau mbele kushughulikia madaktari ili warejee kazini badala ya kuangazia zaidi swala la BBI huku mwananchi akiumia kwa kukosa matibabu.
Story by Wycliffe Sajida