Wakaazi wa wadi ya Chesikaki eneobunge la Mlima Elgon wameshikilia msimamo kuwa kamwe hawatakubali kampuni ya kusambaza maji ya NZOWASCo kusimamia usambazaji maji eneo hilo kwa madai ya kutoa huduma duni.
Wakizungumza kwenye hafla iliyowahusisha wakaazi kutoka wadi ya Chesikaki , bodi ya NZOWASCO na afisi ya utawala ya kaunti ndogo ya Cheptais kutoa maoni kuhusu swala la maji eneo hilo, wamesema tangu NZOWASCO ianze kusambaza maji wamekumbwa na changamoto si haba.
Naye mwakilishi wadi ya Chesikaki Ben Kipkut akihutubu kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa katika afisi ya chifu wa kata ya Chesikaki amehoji kuwa sheria hairuhusu kampuni ya NZOWASCO kuhudumu mashinani.
Aidha Kipkut amesema kwa muda ambao vijana kutoka eneo hilo walisimamia mradi huo changamoto ya maji haikuwa ikishuhudiwa kama ilivyo sasa chini ya uongozi wa NZOWASCO.
Hata hivyo mwenyekiti wa bodi ya NZOWASCO bi Rebecca Masibayi amehoji kuwa sheria imechangia kuwepo huduma duni.
Story by Richard Milimu