Shinikizo zingali zinatolewa kwa serikali na muungano wa kutetea masilahi ya wauguzi nchini kuelewana na kumaliza mgomo ili hali ya matibabu iweze kurejea kama kawaida.

Akizungumza katika mazishi ya Daniel Okanga Olunga ambaye kabla ya kufa kwake alikuwa afisa wa huduma ya afya ya umma katika kaunti ya Nandi kwenye kijiji cha Eluche Mumias Mashariki, mkuu wa huduma ya afya katika kaunti hiyo ya Nandi Alfred Kipchumba amesema kuwa wahudumu wa afya wanatenda kazi kubwa na si vema kwa kusibiwa sikio.

Kipchumba vile vile amewataka wananchi kuwa makini na ugonjwa wa saratani akisema kuwa ni moja wapo wa magonjwa sugu ambayo humaliza watu kutokana na gharama yake ya juu kuudhibiti huku akiwataka kutumia vyakula vya kiasili kujizui nao.

Afisa huyo akisoma ujumbe kutoka kwa waziri wa afya katika kaunti hiyo ya Nandi Rose Koech amemtaja mwendazake Okanga kama mtu aliyekuwa amejitolea kufanya kazi kwa bidii na kuhoji kuwa wataukosa huduma Yake .

Kauli ya mzozo wa wahudumu wa afya kumalizika imeungwa mkono na mwenyekiti wa maendeleo ya akina mama eneo bunge la Matungu aliyehudhuria matanga hayo bi Penina Okechi huku Josia Auther Musita alisema kuwa mgomo wa wauguzi umeleta maafa mengi kwa wananchi wasio na uwezo wa kugharamia matibabu kwenye hospitali za kibnafsi.

Story by Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE