Wakazi wa kaunti ya Kakamega wanaitaka serikali kuu na zile za kaunti kukomesha mabishano na kutafuta suluhu kwa mgomo wa wahudumu wa afya kuepusha vifo

 Wakiongea kwenye mazishi ya mzee Cleophas Okoti katika kijiji cha Makusi wadi ya Butsotso Mashariki Lurambi ambaye alikuwa fundi wa nguo mjini Kakamega, mwenyekiti wa mafundi wa magari mjini Kakamega Moses Musundi amesema vifo vingi mashinani vinatokana na wakazi kukosa matibabu

 Musundi ameitaka serikali kuzingatia maswala ya kuwafaidi wananchi kabla ya kuweka raslimali kwenye ripoti ya BBI

Wakati uo huo msimamizi wa shirika la kijamii la Jisimamie Community Based Organization  linalohusika na maswala ya elimu na miradi ya kilimo katika wadi ya Butsotso Mashariki Cyrus Akhonya amewahimiza wakazi kushirikiana kuendeleza elimu ya watoto chini ya mpango wa jisimamie elimu initiative


Story by Boaz Shitemi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE