Wito umetolewa na viongozi wa wanaoishi na ulemavu kaunti ndogo ya Navakholo kaunti ya Kakamega chini ya mwenyekiti wao Barthez Wechuli kwamba serikali zote za kitaifa na kaunti ziweze kuwajumuisha katika mipangilio ya serikali ili kuona kwamba wanawakilishwa kikamilifu.
Akizungumza na idhaa hii baada ya mkutano wao aliomba serikali kuwashirikisha walemavu katika mipangilio la sivyo wataandaa maandamano.
Aidha, Nicholas Mateba Osendo akiwa mmoja wa viongozi wa wanaoishi na ulemavu kaunti hiyo ndogo ya Navakholo amewarai wazazi wanaoishi na watoto walio na ulemavu waweze kuwapeleka shule ili wapate elimu la sivyo watachukuliwa hatua kali za sheria, pia aliomba walimu pale shuleni wasikue wanawabagua wanafunzi ambao wanaishi na ulemavu.
Story By Tomcliff Makanga