Hali ya taaruki imetanda katika eneo la Konoin katika kaunti ya Bomet, baada ya timbo kuporomoka na kuwazika watu wanne walio kua wanachimba mchanga na kusababisha maafa ya mtu mmoja na wengine watatu kuokolewa
Watatu walio nusurika mmoja alipata majeraha mabaya na kupelekwa katika hospitali ya misheni ya AIC katika kaunti ya Kericho na wawili wametibiwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Chetalal na kuruhusiwa kwenda nyumbani.
Mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 17 alifariki papo hapo baada ya kuangukiwa na kuta za timbo hilo.
Maafisa wa utawala walisema kuwa Emanuel Kirui aliye fariki katika shule ya msingi ya Meswondo alikuwa akiwaongoza marafiki zake katika shughuli hiyo ya kuchimba madini.
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu na wanachama wa kundi la kukabiliana na mikasa nchini wametoa huduma ya kwanza kwa waliojeruhiwa kabla ya kuwapeleka hospitalini.
Story by Imelda Lihavi