Viongozi wa akina mama katika chama cha KANU kaunti ya Kakamega wameshikilia kwamba watatii sheria ambayo itapitishwa bungeni kuhusu swala la wale ambao wanataka kuwania viti mbali mbali kwenye uchaguzi mkuu ujao kuwa na vyeti vya shahada (digrii)

Viongozi hao wakiongozwa na dakta Loice Agoi na Sella Keya, wanasema kuwa kama chama hawana nia ya kutenda kinyume cha sheria za humu nchini na iwapo sheria hiyo itapitishwa kivyovyote vile wataiunga mkono kikamilifu

Viongozi hao waliyasema haya kwenye mkutano wao Shibuli eneo bunge la Lurambi ambapo wameanzisha mchakato mzima katika kaunti ya Kakamega wa kuwasajili wanachama katika chama cha KANU, wakiwarai wakaazi wa magharibi kukikumbatia chama hicho

Aidha wamewataka akina mama kijitokeza kwa wingi na kuwania nyadhfa mbali mbali za kisiasa kipitia kwa chama hicho

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE